Jane's Journey

Home » Casts » Lucy Komba


Lucy Komba

Other Name/s: Lucy Francis Komba

Date/s: 24 October 1980

Actor | Director | Film Writer | Producer

Lucy Francis Komba (amezaliwa tar. 24 Oktoba, 1980) ni mwigizaji wa filamu, mwongozaji na mtayarishaji kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha filamu ya Yolanda 1-2 na Utata. Lucy pia ni mmoja kati ya waliokuwa waigizaji wa kundi la sanaa la Kaole Sanaa Group.

Lucy Francis Komba

Maisha ya Awali
Lucy Francis Komba alizaliwa mnamo tarehe 24 Oktoba ya mwaka wa 1980, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alipata elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Peters Nusery School na msingi alisoma katika shule ya Oysterbay Primary School. Elimu ya sekondari alisoma Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro, kwa kidato cha 1 - 4 na 5 - 6 alisoma katika shule ya Kibosho Secondary School.
Kwa elimu ya vyuo, alisoma katika Chuo cha Utumishi wa Serikali na alisomea maswala ya IT (Information Technology) na alipata Diploma katika elimu hiyo.

Sanaa ya Awali
Lucy Komba alianza maswala ya sanaa katika kundi la sanaa la Fukuto Arts Professional. Akiwa huko alishiriki katika baadhi ya mifululizo ya vipindi vya televisheni kama vile “Valentine Day”  na “Rangi ya Chungwa” Baada ya hapo akaelekea zake katika kikundi cha Dar Talent, akiwa huko alipata kushiriki katika filamu moja ya vichekesho. Baada ya hapo alilekea zake katika kikundi cha sanaa cha Kaole Sanaa Group, akiwa huko alipata kushiriki katika mifululizo minne ya vipindi vya televisheni (tamthilia).

Kazi Binafsi
Baada ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za uigizaji, Lucy akaamua kufanya kazi zake mwenyewe, yaani kutayarisha, kutunga, kuongoza inakuwa chini yake. Akiwa anamiliki kazi zake mwenyewe, Lucy alianza kutayarisha filamu ya kwanza kabisa ni ile ya “Utata” na ya pili ni “Yolanda” sehemu ya kwanza na ya pili, Vice Versa na Ama Zako Ama Zangu. Mbali na kucheza filamu zake, Lucy pia ameshiriki katika baadhi ya filamu nyingi tu za Tanzania.

Kama Mwigizaji
- Division of Love
- Jelaha la Ndoa
- Taraka Wodini
- Siri ya Moyo Wangu
- Teke la Mama
- Swadakta
- Richmond

Kama mtayarishaji/mtunzi/mwigizaji
- Utata
- Yolanda 1 - 2
- Vice Versa
- Ama Zako Ama Zangu

Email: lucy_komba@yahoo.com

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Lucy Komba
  • Twitter Page of Lucy Komba
  • YouTube of Lucy Komba
  • Website of Lucy Komba
Source: https://lucykomba.com/
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More