Home » Highlights » Tamthilia ya Siri ya Mtungi Yazinduliwa Jijini Dar Es Salaam


Tamthilia ya Siri ya Mtungi Yazinduliwa Jijini Dar Es Salaam

Posted: 06 Dec, 2012

Mchanganyiko mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa, au kwa mapenzi tu, unaunda jamii inayohamasishwa na penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha, na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki.

Siri ya Mtungi Launch 01
Louise Kamin Meneja Mradi wa Media For Development International Tanzania akizungmza kuelezea filamu ya Siri ya Mtungi ilyotengenezwa na taasisi hiyo itakayokuwa ilirushwa na vituo vya televisheni vya ITV na EATV ikiwa na maudhui ya maisa katika familia ya jamii inayohamasishwa na penzi,  lililoletwa na woga,  ushirikina na usaliti,  ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha,  na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki. Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika jana kwenye ofisi za shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam

Siri ya Mtungi Launch 02
Baadhi ya waandishi wa habari na wageni walioalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam.

Siri ya Mtungi Launch 03
Baadhi ya washiriki waliocheza katika filamu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo jana.

Tamthilia mpya kabisa ya Televisheni kutoka kwa Watu wa Marekani!  Onyesho la Kwanza la SIRI YA MTUNGI litakuwa ITV saa 3.30 usiku tarehe 9 Desemba.  Na EATV saa 3.30 usiku tarehe 12 Desemba.

Mchanganyiko mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi,  waliohusiana kwa damu au ndoa,  au kwa mapenzi tu,  unaunda jamii inayohamasishwa na penzi,  lililoletwa na woga,  ushirikina na usaliti,  ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha,  na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki. 

Tamthilia hii ya Televisheni ni Programu ya   awali ya TCCP (Tanzania Communications Capacity Project)  iliyotekelezwa na JHU-­‐CCP (Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communications Programs)  kwa msaada wa USAID (United States Agency for International Development)  na kama sehemu ya PEPFAR (US President’s Emergency Fund for AIDS Relief). 

Ikiwa imetayarishwa na MFDI (Media For Development International),  Siri ya Mtungi inawaleta pamoja Wasanii bora wa Tanzania,  waandishi,  wana mitindo ya nguo,  wakurugenzi wa sanaa,  waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania. 

Kati ya mitaa yenye harakati nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya Bagamoyo,  tunapenya nyuma ya milango iliyofungwa mpaka kwenye maisha ya Cheche na mkewe Cheusi,  binti wa kiongozi maarufu katika jamii,  mwenye wake wengi,  Mzee Kizito,  pamoja na wahusika wengine kama Duma,  mwana DJ;  Lulu-­‐  shangingi lililokubuhu;  Farida-­‐ 
roho ya nyoka;  Masharubu-­‐  mzee kikwekwe na wengine wengi.     

RATIBA YA ITV:  Jumapili 3.30 usiku -­‐  Jumatano 3.30 usiku
RATIBA YA EATV:  Jumatano 10.30 Alasiri   -­‐  Alhamisi 7.00 Mchana -­‐  Jumamosi 10.30 Alasiri

Reviews / Comments

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More