Home » Highlights » Watanzania Washiriki Kwenye Filamu ya Lost In Abroad Nchini Marekani


Watanzania Washiriki Kwenye Filamu ya Lost In Abroad Nchini Marekani

Posted: 05 Apr, 2012

Raia wawili wa Tanzania ambao ni wakazi wa jijini Dallas nchini Marekani wameshiriki katika filamu mpya itakayotoka karibuni iitwayo "Lost In Abroad".

Sitti Mtemvu akiwa na Itika Mwakasula ndani ya Dallas

Watanzania hao wawili ni Itika Mwakasula na Sitti Mtemvu ambao wote ni wakazi wa jiji la Dallas katika jimbo la Texas nchini Marekani wameweza kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwa kuigiza kwa umahiri mkubwa katika filamu hii mpya ambayo ni ya kuvutia.

Filamu hiyo ambayo imeshirikisha waigizaji mbalimbali kutoka nchi nyingine nyingi za Kiafrika imeongozwa na Chijindu Kelechi Eke kutoka nchini Nigeria ambaye pia ndio muigizaji mkuu.

Filamu hiyo inayozungumzia uhamiaji wa Waafrika kwenda nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya masomo na ubora wa elimu huku wakiwa na matumaini ya kurudi kwenye nchi zao lakini matokeo yake wengi wao huamua kubakia kwenye nchi hizo husika kutokana na ubora wa maisha.

Suala hili la Waafrika kuamua kubakia ughaibuni ambapo wakati mwingine huwa ni tatizo kubwa kwao hasa kutokana na kutozoea tamaduni mpya za ughaibuni ambazo ni tofauti kabisa na tamaduni za Kiafrika.

Filamu hiyo pia inaangalia ni jinsi gani Waafrika wanaweza kuishi ughaibuni huku wakilea watoto wao kwa kutumia desturi za Kiafrika huku pia wakichanganya na tamaduni chanya za ughaibuni na pia kutosahau asili yao.

Filamu hiyo itaanza kuonyeshwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 25 Februari 2012 katika ukumbi wa Majestic Theatre jijini Dallas nchini Marekani.

 

 

More Photos

Reviews / Comments

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More