SKU: DT461 | DVD I | Year -
Christina Shusho - Nipe Macho (CD)
1. Nina Wimbo
2. Bado Nakungoja
3. Mungu Uhimidiwe
4. Nipe Macho
5. mapito
6. Mungu Akiwa
7. Thamani ya Wokovu
8. Ni Kwa Neema
9. Ushirika na Roho
10. Mungu wa Huruma
Wote tunapitia mambo mengi katika Maisha. Albu yangu hii leo ni ya pekee kwa njia nyingi, ni safari ya maisha ambayo hatuwezi kuepuka. Mimi binafsi ninamshukuru Mungu kwani
Nina Wimbo katika Maisha yangu. Hapo Mwanzo Mungu aliptuumba alituanzishia safari ya maisha. Ninafurahi kusema Mungu Uhimidiwe kwani unastahili.
Safari hii ya maisha ina mambo mengi na misukosuko kwa kila mtu, nimelazimika kumwambia Mungu Nipe Macho nione yanayotukia katika safari hii.
Nimeona ktk shida na furaha Mungu ameandaa Mapito mengi. ktk Mapito haya tunahitaji kutambua kwamba kila jambo linawezekana Mungu akiwa Upande wetu. Uwepo wa Mungu ktk safari hii ya maisha umedhirishwa namambo kadhaa aliyopanga Mungu juu yangu, kwa ajili ya Thamani ya Wokovu wangu, na kwa jinsi ambavyo Ni Kwa Neema Nimekombolewa na ninapata hamu kubwa ya kuwa na Ushirika na Roho Mtakatifu usiozurika, Ushirika endelevu.
Ni ktk mtazamo huu ndipo naona safari yangu inajawa na shukrani nyingi ninapotambua Mungu amejaa Huruma zinazo niwezesha ktk safari. Ninakukaribisha ushereheke nami ktk furaha hii ya Kuwa na Wimbo