Jane's Journey

Home » Casts » Khadija Kopa


Khadija Kopa

Other Name/s: Khadija Omar Abdallah Kopa - Gwiji wa Taarab / Malkia wa Mipasho

Entrepreneur | Singer | Song Writter

Khadija Omar Abdallah Kopa, Gwiji wa Taarab

Khadija Kopa anasema alizaliwa mwaka 1963 kisiwani Zanzibar na ni mtoto wa kipekee katika familia ya Kopa. Nimeolewa na nina watoto wanne na wajukuu wawili.

Kazi ya sanaa alianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical Club.

Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia mwanaharakati wa kisiasa kwao nyumbani Tanzania.

Mama huyu alipata sifa zaidi kutokana na uimbaji. Lakini si wengi wanaojua kuwa ni kipawa alichozaliwa nacho.

Khadija alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo, akisomea madrasa Zanzibar.

Nikiwa chuoni (madrasa) nilikuwa msomaji mzuri wa qaswida, halafu vilevile nilipokuwa Young Pioneer, nilikuwa kwenye kikundi cha kwaya, anasema.

Shuleni vilevile nilikuwa kwenye mambo ya ngoma, mambo ya utamaduni na kwaya. Shule yetu ilikuwa ni bingwa kwa kwaya Zanzibar. Niliendelea hivyo hadi katika shule ya upili.

Siku moja nilikuwa nimekaa nikiiga wimbo. Akapita babu yangu aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akaniambia najua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuniandikia barua mwenyewe bila kunishauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba nijiunge nao.

Akishirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir, marehemu Leila Khatib na wanaume kama Abdul Misambano na Ali Star, waliporomosha nyimbo ambazo zitasalia milele masikioni mwa wapenzi wa taarab.

Kwa miaka zaidi ya 11 sasa, Kopa ameendelea kuporomosha muziki na sauti yake ile ile isiyokwisha utamu katika kundi la Tanzania One Theater TOT Taarab na vilevile ameimmbia vikundi vingi sana.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Khadija Kopa
  • Twitter Page of Khadija Kopa
  • YouTube of Khadija Kopa
  • Website of Khadija Kopa
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More