Home » Highlights » Bi Kidude Atunukiwa Nishani na Rais Kikwete katika sherehe za Uhuru
Bi Kidude Atunukiwa Nishani na Rais Kikwete katika sherehe za Uhuru
Posted: 11 Dec, 2012Katika kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanzania jana Rais Jakaya Kikwete amemtunuku Nishani ya Sanaa na Michezo muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Bibi Fatma Binti Baraka Khamis
(Bi. Kidude) kwa mchango wa kipekee kwa taifa la Tanzania katika nyanja ya sanaa.
Pamoja na Bi. Kidude, watu wengine katika makundi mbalimbali wametunikiwa nishani za heshima katika halfa iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu
Rais Kikwete akimvisha Nishani ya Sanaa na Michezo Bi Kidude
Rais Kikwete akimpongeza mara baada ya kumpa Nishani ya Sanaa na Michezo Bi Kidude