Home » Highlights » Juma Kolowoko Sajuki achangiwa Sh. mil 16 kwenda India


Juma Kolowoko Sajuki achangiwa Sh. mil 16 kwenda India

Posted: 10 May, 2012

Msanii nyota wa filamu anayesumbuliwa na uvimbe tumboni, Juma Kilowoko `Sajuki'` Safari ya msanii nyota wa filamu anayesumbuliwa na uvimbe tumboni, Juma Kilowoko 'Sajuki' ya kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu imeiva, baada ya wasamaria wema kumchangia kiasi cha Sh. milioni 16.

Juma Kolowoko Sajuki

Japo fedha hizo ni pungufu ya Sh. milioni 9 ya fedha zote zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya safari ya msanii huyo kwenda nchini humo kutibiwa, lakini mkewe Wastara Juma ameshukuru kwa sababu inamwezesha mumewe kusafiri.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio, Wastara, alisema anawashukuru watu wote waliofanikisha kupatikana kwa fedha hizo pamoja na tiketi tatu za ndege za kumsafirisha mgonjwa, yeye na kaka wa Sajuki kwenye matibabu hayo.

“Kwa kweli nawashukuru watu wote waliojitolea kwa hali na mali kumsaidia mume wangu kwani nimefanikiwa kupata Sh. milioni 16 kati ya Sh. milioni 25 zilizokuwa zikihitajika,” alisema.

Aliongeza kutokana na kupatikana kwa fedha hizo huenda wakaondoka nchini kwenda India kwenye matibabu kati ya Jumapili au Jumatatu ijayo.

“Nadhani kati ya Jumatatu au Jumapili ijayo tunaweza kusafiri ambapo mbali na Sajuki mwenyewe, kwenye msafara nitakuwepo na mimi na kaka wa Sajuki,” alisema.
Hata hivyo Wastara alinukuliwa akilia na watu waliomliza kiasi cha Sh. 800,000 katika akaunti yake ya simu iliyokuwa ikitumiwa kuchangishia fedha hizo, ingawa anaendelea kuzifuatilia katika makao makuu ya mtandao huo wa simu za mikononi.UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ anaumwa, Ijumaa limemshuhudia na linakuhabarisha.

Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.

Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.

WASANII WAMTOLEA MACHOZI
Kabla ya kuugua, Sajuki alikuwa mwanaume aliyeshiba (mnene) na mwenye nguvu hivyo kutokana na hali yake ilivyobadilika na mwili kuwa mdogo, baadhi ya wasanii waliofika kwenye sherehe hiyo walijikuta wakimtolea machozi.
“Jamani tuacheni utani, Sajuki anaumwa sana na anahitaji msaada na maombi yetu ili arejee kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa waigizaji wenzake.

SAJUKI KURUDI INDIA
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

 

Reviews / Comments

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More