Jane's Journey

Home » Casts » Adam Kuambiana


Adam Kuambiana

Other Name/s: Adam Philip Kuambiana

Date/s: 06 June 1976 - 17 May 2014

Actor | Director | Film Writer

Adam Philip Kuambiana alizaliwa mwaka 1976 Ifunga Mkoani Iringa, alipata elimuya msingi katika shule ya Mlimani Jijini Dar nabaade sekondari ya Tambaza kisha akahamia jijini Nairobi kwenda kusoma kidato cha tano nasita baada ya hapo alielekea Afrika Kusini kupata elimu ya filamu na baada hapo alikuwa fiti katika uwigizaji, uongozaji na pia alikuwa mwandishi wa miswada ya filamu.

Adam Kuambiana

Miongoni mwa filamu ambazo ametia mikono yake kwa kiwango kikubwa ni pamoja na Fake Pastor, Life of Sandra, Danija, Regina, Faith, More Fire, Scola, Lost Son, My Fiance, Jessica, Basilisa, Nobody, Chaguo Langu na nyingine nyingi.

KAMA ni mpenzi wa filamu Bongo basi unaposikia jina la Adam Philip Kuambiana si jina geni midomoni na hata masikioni mwao, historia ya kijana huyo wa Kihehe ilifunguka pale alipoigiza filamu ya kwanza iliyojulikana kwa jina Fake Pastor iliyoandaliwa na mkurugenzi wa Global Publishers ya jijini Dar es Salaam hapo ndipo Mtwa Kuambiana nyota ilipowaka.

Kwa sasa Adam Kuambiana inapendeza ukimwita Director Adam Kuambiana kutokana na umahiri wake wa kuongoza filamu kali na za kusisimua hata kumfanya ale shavu katika kampuni bora ya utengenezaji wa filamu Bongo kama si Afrika Mashariki kampuni hiyo si nyingine bali ni RJ Company inayongozwa na gwiji la filamu Swahilihood.

Ukiondoa fani yake ya uigizaji ambayo ndio ajira yake rasmi katika kuonyesha kuwa yeye ni mbunifu na msanii mwenye kujenga kitu kipya ambacho kila mtu anaweza kujisikia kukifanya na kuwa mfano wa kuigwa na wengine, basi Director Kuambiana amekuja na staili mpya kabisa ya muonekano wa nywele zake na ndevu zikionyesha rangi nyeupe.

Huku akionyesha ukakamavu kwa sababu kuwa ni mtu wa mazoezi, kwangu nimefurahia muonekano huo kwani ni sehemu ya sanaa na amefanya kile ambacho angeweza kumfanyia mwigizaji na kubadilika kuwa mtu mwingine kabisa.

Huyo ndio Director Adamu Kuambiana akiwa kama Mzee Jangala hivi au ukipenda unaweza kumuita Mh. Lowasa yote heri kimsingi utakuwa umemtendea haki kwa kuonyesha kitu cha kipekee katika dunia ya ubunifu kutoka kwake Hongera zake.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Adam Kuambiana
  • Twitter Page of Adam Kuambiana
  • YouTube of Adam Kuambiana
  • Website of Adam Kuambiana
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More