Jane's Journey

Home » Casts » Flora Mbasha


Flora Mbasha

Other Name/s: Flora J. Mayalah

Date/s: 01 June 1983

Singer | Song Writter

Nilizaliwa tarehe 1st June 1983 katika hospitali ya Hindu Mandhal mjini Mwanza. Baba yangu anaitwa Henry Joseph Mayalah ambaye kwa sasa ni marehemu. Mama yangu anaitwa Calorin Moses Kulola. Katika familia yetu tumezaliwa watoto wa 5, wa kiume ni mmoja aitwaye Benjamini na wakike tupo wa nne, mimi nikiwa wa pili kuzaliwa, akafuata Dorcus, Suzan na wa Mwisho akiwa ni Esther.

Flora E. Mbasha

Sisi ni Wasukuma wa Sengerema wilaya ambayo imo ndani ya mkoa wa Mwanza. Nimekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, babu yangu akiwa ni Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assembilies of God. Babu na bibi yangu mpenzi Elizabeth ndiyo walionilea kwa pamoja wakishirikiana na mama yangu mpendwa.

Nilianza kuimba nikiwa darasa la tatu. Wakati huo nilikuwa nikienda na mama zangu wadogo kwaya hadi nilipokuwa na miaka kumi na tatu na ndipo nilipoanza kushiriki kuimba kwaya kanisani na kuimbisha baadhi ya nyimbo.

Baada ya kufunga ndoa mwaka 2002/9/22 tulianza kuimba pamoja na mume wangu tukiwa na Word Alive Band. Mungu alitunisaidia mwaka 2003/6/ nikajifungua binti mrembo aitwae Elizabeth, jambo hili hunifanya nimshukuru Mungu kwa kutupa mtoto kila wakati. Mwaka wa 2004 nilifanikiwa kurekodi album yangu ya kwanza niliyoita “JIPE MOYO” ikiwa na nyimbo 10.

Nyimbo zote hizi tuliimba pamoja kwa kushirikiana na mume wangu mpenzi Mr. Emmanuel Mbasha ambaye kwa kweli amekuwa msaada mkubwa sana katika huduma ambayo Mungu ameiweka ndani yangu.

Baada ya album yangu ya kwanza ya “JIPE MOYO” tulifanikiwa kutoa Albam ya pili niliyoiita “UNIFICHE” ambayo nayo ilikuwa na nyimbo 8. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kwa kila hatua niliyofanya.

Nilifanikiwa pia kutoa albamu yangu ya tatu inayoitwa “FURAHA YAKO” yenye nyimbo 12 ambazo ni

Namshukuru Mungu kwa kuwa alimtoa yesu akafa kwa ajili yangu kwani kwa kipingwa kwake mimi Flora ninaweza kuimba kumsifu Mungu kwa naama yeyote ile na kama si Yesu kujitoa msalabani kwa ajili yetu sisi wote wanadamu, sijui ningekuwa wapi sasa.

Sifa na utukufu namrudishia Mungu kwani ndiye mweza wa vyote mbingu na nchi ameziumba, wanyama na wadudu, miti na vitu vyote viliyomo ndani ya dunia na mbingu ameumba yeye, bila kusahau binadamu ambaye ameumbwa akiwa na akili kuliko viumbe vingine vyote. Kweli Mungu ni Mungu Mwacheni Mungu aitwe Mungu.

Tumeshafanya huduma sehemu mbali mbali ikiwemo mikutano ya injili na matamasha ya dini na ya kijamii. Pia tumeimba katika kampeni za kugombea Urais Raisi za Mhe. Jakaya Kikwete za chama cha Mapinduzi. Tulishiriki katika mikoa ya kanda ya ziwa kama waimbaji na tunamshukuru Mungu kwa kuwa alitupigania.

Pia tuliweza kuzunguka sehemu mbalimbali na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, na moja ya sehemu tulizokwenda kuimba ni katika daraja linalounganisha Msumbiji na Tanzania.

Tunamshukuru sana Mungu kwa matamasha mengi na ya Injili ambayo tumeshayafanya. Tamasha la Inili la ufunguzi wa album yanguya kwanza lilivunja Rekodi ya matamasha mengine yote ya injili tulowahi kufanya.

Tamasha hili lilifanyika mkoani Kilimanjaro, kwenye viwanja vya Hindu Mandhal vinavyotazamana na kituo kikuu cha mabasi, mjini Moshi. Watu walifuka hata mahali pa kukanyaga hapakuonekana, walikuwa ni wengi haikuwahi kutokea awali. Lilikuwa ni tamasha lenye mafanikio sana na tunamshukuru sana Mungu kwa kutufanikishia tamasha hili.

Hivi sasa kunatambulisha album yetu ya tatu inayoitwa “FURAHA YAKO”. Kwa kila ziara zetu, kila tunakokwenda huwa ni kawaida yetu kuchangia na kutoa misaada kwa vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya watu wanaoishi katika mazingira magumu, hasa watoto yatima. Tunatambua pia kuna walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa, hivyo hatuwezi kuachia serikali pekee yake. Hao pia huwa wanapata kila ambacho tumepanga kuwagawia. Hata Hivyo inabidi watu wote tushirikiane ili kuwasaidia ndugu zetu walemavu ambao hawakupenda kuwa kama walivyo, na tukumbuke kuwa hujafa hujaumbika na biblia inasema sadaka iliyo safi ni kuwasaidia yatima na wajane.

Mimi Flora na mume wangu Mbasha tunaamini kuwa kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu ni kuwatengnezea njia nuru watoto wetu.

Hivyo ni vizuri kuwakumbuka ndugu zetu walemavu hawa kwa chochote tulicho nacho na unaweze kupeleka katika kituo chochote kinachotoa msaada kwa ndugu zetu walemavu hawa kwani vipo kila sehemu nchini mwetu.

Malengo yetu kwa sasa ni kufungua studio yetu wenyewe na kununua vyombo vitakavyotuwezesha kupiga muziki “LIVE” na sio kuimba kwa kufuatia nyimbo ilopigwa tayari (Playback (CD)) kama tufanyavyo kwa sasa.

“Flora Mbasha” ni kundi la waimbaji tunalo liongoza sisi wenyewe na kwa msaada wa watu wachache wenye moyo wa kutusaidia huduma yetu ili izidi kusonga mbele.

Ili kuweza kukamilisha malengo yetu, tunahitaji msaada mkubwa kutoka kwenu, ninyi wapenzi wa muziki wa injili ili tuweze kununua kununua vyombo vitakavyotuwezesha kupiga muziki “LIVE”. Vyombo hivi kwa kweli vina gharama kubwa,  hivyo basi tunakuomba, ikiwa ungependa kutusaidia chochote ambacho Mungu atakuwezesha, waweza kuwasiliana nasi, kwani naamini kwa kutusaidia “Flora Mbasha” Team utakuwa unazitafuta baraka zaidi za Mungu na ninamini kabisa Mungu atakubariki na kukuzidishia zaidi.

“Flora Mbasha” Team hatuimbi kama burudani nyingine ila tunaihuburi injili kwa njia ya nyimbo ili watu wengi wawe wakipona, wakipata faraja, wakifanikiwa, kupitia huduma yetu ambayo Mungu kaweka ndani yangu.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Flora Mbasha
  • Twitter Page of Flora Mbasha
  • YouTube of Flora Mbasha
  • Website of Flora Mbasha
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More