Jane's Journey

Home » Casts » H Baba


H Baba

Other Name/s: Hamisi Ramadhani Baba a.k.a H Baba

Actor | Singer

H baba ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1987 mkoani mwanza anaeleza kuwa licha ya muziki huu wa kizazi kipya kufanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati bado kunatatizo la wasanii kutambua majukumu yao katika jamii inayowazunguka.

Hamisi Ramadhani Baba a.k.a H Baba

H BABA
H baba wasanii tujitambue sisi kwanza

Msanii anaofanya vizuri jukwaani katika mtindo wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini utasita kumtaja kijana kutoka mkoa wa Mwanza Hamisi Ramadhani(H baba) kutokana na staili yake ya potezapoteza.

H baba ambaye kila siku anatembea na falsafa kuwa mama ndio chanzo cha mambo yote hivyo anahakikisha mapato anayopata anagawa nusukwanusu na kumpelekea mama yake.

Anasema kuwa hali hiyo ilishindwa kueleweka mara baada kutakiwa na timu ya Azam kwani alihitaji kiasi cha shilingi milioni ishirini ikiwa kumi kwa mama na kumi kwake yeye lakini walishindana kutokana na kiasi hicho kuonekana kuwa kikubwa.

Baada hapo ndipo aliamua kujikita zaidi katika muziki wa Bongofleva ambao ndio sehemu yake ya maisha na anafanya muziki kuwa ndio chaguo la kwanza la kuingiza mapato katika maisha yake ya kila siku.

Anasema licha ya muziki huu kuonekana kuwa unamafanikio makubwa kwa wasanii wenyewe na hata kupenya katika jamii kwa kasi kubwa lakini bado mafanikio yake sio kama vile yalivyo katika hisia za wapenzi wa muziki huu.

Anaeleza kuwa muziki huu umepungua chati kwa sasa kutokana na bahadhi ya watu waliopo katika tasnia hii kuhodhi muziki huu kama wa kwao hali inayo hatarisha ustawi wa wanamuziki wa kweli na wasisi wa muziki huu.

Anaeleza moja ya chanagamoto wanazo kumbana na nayo wasanii wamuziki huu ni malipo duni ambayo yanatolewa na mapromota ambao ni matapeli wa maneno na kuwasainisha mkataba feki wasanii.

“Hali ilivyo katika muziki hapa nchini ni mbaya kwani wasanii awajitambui na wamekuwa watu wakudhulumiwa kila siku kama mimi ninavyokueleza albamu yangu ya mpenzi bubu sijalamba hata shilingi kumi zaidi ya propaganda"alisema H baba.

Anaeleza kuwa changamoto nyingine wanayopata wasanii wa hapa nchi ni hile matamasha ya kimataifa yanayo andaliwa nchini kutotoa kipaumbele kwa wasanii wanaoweza kufanya vizuri na kuchagua kwa kujuana hali inayo shusha muziki wetu kwa wageni.

Anaeleza kuwa hata vyombo vya habari vya ndani vimeshindwa kutoa thamani kwa msanii wa nyumbani pindi kazi yake inapoibiwa na kusapoti mwizi wa kigeni.

“ninathubutu kusema kuwa nyimbo inayowika sasa hivi ya Abha Prakatatumba ni kopi ya wimbo wangu wa mpenzi bubu ambao ulitoka miaka mitatu iliyopita lakini leo watu wamekopi sisi nyumbani tunaona kitu kipya"alisema H baba.

Anasema kuwa wasanii wengi wa kitanzania sio wabunifu katika utunzi hali inayo hatarisha ustawi wa muziki huu ambao tunaita wa kizazi kipya kwa ni karibu wasanii wote wanaimba mada moja.

Anaeleza kuwa ni vema wasanii wakawa wachambuzi na watafaiti wa mada mbalimbali zinazo igusa jamii hili waweze kutumia muziki huu kuelimisha umma unao tuzunguka.

Anaelezakuwa kutokana na hali hiyo ameamua kuja na staili mpya inayokwenada kwajina la Bongo Bolingo Fleva ambayo anamini itampa sura mpya katika muziki huu whuko tunako elekea.

Anasema kuwa lengo la kufanya mtindo huo wa bongo bolingo ni kuhakikisha kuwa anafanikiwa kuteka soko la Afrika Magharibi na ufaransa ambako bolingo inapendwa.

Anasema kuwa umahairi wake wa kutumbuiza kwa uhakika kwa muda wa masaa matatu kitakuwa moja ya kigezo kitakacho wavutia wapenzi wake wamataifa hayo mapya pindi ataka[po penya kutumbuiza.

Anasema kuwa yeye ndio msanii pekee Afrika Mashariki aliyeweza kuvunja rekodi ya msanii kutoka Uganda Joseph Camerion kwa kufanikiwa kufanya show kwa muda wa saa tatu akimzidi mganda huyo nusu saa.

Anaeleza kuwa yeye kama yeye sasa ametanuka kisanaa na ategemei sanaa ya muziki pke yake kwani sasa anakairi uwezo wake wa kufanya filamu umeongezeka kwa kasi kubwa kuliko hapo awali kwani amepata kushirikishwa filamu nyingi sana na zimefanya vizuri sokoni.

H baba ambaye ni mtoto pekee katika tumbo la mama yake anaeleza kuwa katika maisha yake ya kila siku yupo tofauti na watu wengine kwani atumiii kilevi cha aina yoyote na ana mpenzi mmoja ambaye ni mchumba wake anayefahamika kwa jina la Frola mvungi.

Anasema kuwa kama msanii unajieshimu na unajua nini unafanya unafasi ya kuficha mchumba wako ninani kama unaficha basi ujue kuna walakini katika mwenendo wako wa kila siku.

Anasema kuwa yeye amekuwa akiishi maisha ya kawaida sana kiasi cha kusema kuwa anashangaa watu ambao wamejiunga katika mtandao wa Face book kwa ajili kufanya ufuska hali iliyomfanya yeye kuchukia mtandao huo.

Nakama kuna kitu ujui kuhusu mimi mimi sipendi kwenda klabu ukinikuta klabu ujue siku hiyo hapo ninashoo kwani nahisikkwenda klabu nitapoteza heshima yangu na kujishusha mwenyewe.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of H Baba
  • Twitter Page of H Baba
  • YouTube of H Baba
  • Website of H Baba
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More