Jane's Journey

Home » Casts » Ndumbagwe Misayo “Thea”


Ndumbagwe Misayo “Thea”

Other Name/s: Ndumbagwe / Ndubangwe Misayo a.k.a "Thea"

Date/s: 06 November 1982

Actor | Director | Producer

Ndumbagwe Misayo, Thea, mtoto wa kwanza katika familia ya Matilda Misayo na Gaudence Urassa, alizaliwa mwaka 1982 mkoani Shinyanga, kabla ya kuhamia Dar es Salaam na wazazi wake, ambako alipata elimu ya Msingi katika shule ya Mapambano, Sinza na baadaye kujiunga na sekondari ya Zanaki, alikosoma hadi Kidato cha Tatu kabla ya kuhamia Greens Victoria, alikohitimu kidato cha Nne mwaka 2001.

Ndumbagwe Misayo "Thea"

The anasema sanaa ya uigizaji ilikuwa kwenye damu yake tangu angali binti mdogo anasoma darasa la tano, alipokuwa akishiriki kwenye kikundi mcha sanaa cha shule na pia katika Kanisa Katoliki la Mwananyamala.

Akiwa kidato cha kwanza tu, Thea anasema alikwenda kujiunga na kikundi cha Mambo Hayo ambako hata hivyo baada ya kundi kusambaratika, akahamia Kaole.

Anawataja wasanii waliomvutia zaidi siku za mwanzoni kwamba walikuwa ni Suzanne Lewis anayejulikana kwa jina la sanaa kama Natasha, Jacob Steven au JB ambaye siku hizi anataka aitwe Amitabh Buchan wa Tanzania na wengineo.

Anakumbuka igizo lake la mwisho kucheza kundi la Kaole lilikuwa ni Baragumu mwaka 2005, alipoigiza kama mke wa mwanasiasa Mzee Magari, ambaye baadaye ankutana na kijana mkimbizi, Kanumba. “Yaani humo na mimi historia yangu inakuwa kama ni mkimbizi pia, kwa sababu naye Kanumba alikuwa mkimbizi mimi nikaamua kumsaidia, lakini mume wangu sasa, Mzee Magari akawa hapendi. akawa anafanya njama za kumfunga bila kujua kwamba alikuwa ni mtoto wake,”anasema.

Anataja baadhi ya filamu alizocheza hadi sasa ukiondoa By One na Bed Rest, kuwa ni Dadaz, Ukungu, Dunia Yangu, Revenge, Sigito, Tone la Damu, Why Me, Solemba, Born To Suffer, Simanzi ya Moyo, Trip To America na Out of Love.

Mshindi huyo wa tuzo ya Vinara mwaka 2008 kama mwigizaji bora wa kike, ni mama wa motto aitwaye Marlow Mpera, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Diamond, Dar es Salaam.

Anazungumzia kupanuka kwa soko la filamu nchini kwa kusema kwamba, wasanii wanapaswa kuitumia vizuri fursa hiyo kwa kufanyaq kazi nzuri, ili waweze kuvutia wapenzi wengi. “Tukifanya kazi ili mradi tu iingie sokoni tupate fedha kwa sababu tuna majina makubwa, tutaharibu mambo,”anasema.

WASIFU WAKE:
JINA: Ndumbagwe Misayo
JINA LA UTANI: Thea
KUZALIWA: 1982
ALIPOZALIWA: Shinyanga
SANAA: Uigizaji

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Ndumbagwe Misayo “Thea”
  • Twitter Page of Ndumbagwe Misayo “Thea”
  • YouTube of Ndumbagwe Misayo “Thea”
  • Website of Ndumbagwe Misayo “Thea”
 
 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More