Jane's Journey

Home » Casts » Riyama Ally


Riyama Ally

Other Name/s: Riyama Ali

Actor | Film Writer | Producer

Riyama Ally

Riyama Ally ni msanii wa maigizo tangu mwaka 2000 wakati huo akiwa kwenye kundi la sanaa la Taswira ambaye ,anasema , hatasahau siku yake ya kwanza kuona matunda ya sanaa yake baada ya kuigiza vyema kama mtoto aliyegeuzwa kichaa na mama yake ambaye alichanganya dawa alizopewa na mganga ili ampe baba yake. Nafasi hiyo aliicheza katika tamthilia ya ‘Jabari’ iliyokuwa ikionyeshwa na kituo cha luninga cha ITV.

Riyama anasema ilipofika mwaka 2003 alijiunga na kundi la sanaa la Tamba Art Group lililokuwa likizalisha filamu za kiswahili kama ‘Miwani ya Maisha’, ‘Mzee wa Busara’ na nyinginezo nyingi ambapo yeye alicheza kwenye filamu za ‘Nsyuka’ na ‘Fungu la Kukosa’ ambazo pia ni miongoni mwa filamu zilizoandaliwa na kundi hilo.Riyama anasema mbali na filamu zinazozalishwa na kundi hilo, pia amecheza kwenye filamu nyinginezo za nje ya kundi kama ‘My Darling’ kutoka kundi la White Elephant, na akacheza pia kwenye filamu za simu ya kifo, Darkness Night, Mwana pango , Kolelo na Segito’.Kwa sasa Riyama anatarajia kuonekana tena kwenye filamu yake mwenyewe itakayoitwa ‘Mwasu’, yeye akicheza kama mhusika mkuu ambaye ataonekana kama msichana aliyelelewa katika maisha ya kitajiri lakini akajikuta akijiunga na genge la wabwia unga, madawa ya kulevya na kufanya maasi makubwa hata kuua na kupelekwa jela. 

”Hii ni baada ya wazazi wangu kuhitilafiana na kutengana hivyo mali zikasambaratika na kuwa hatuna mbele wala nyuma”, anasema Riyama.Riyama anasema pia ni mtunzi wa hadithi mbali mbali za filamu moja wapo ikiwa ni hiyo yake ya ‘Mwasu’ na nyingine ambayo ameiuzia kampuni ya CB ya Charles Mokiwa, ilioko Uingereza.

Kila la kheri Riyama sisi tunakukubali na ndio kinara wetu katika safu ya uigizaji bora hadi sasa huna mpinzani kaza buti na sio kwamba tunabisha hawa waliochaguliwa lakini habari ndio hiyooooo

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Riyama Ally
  • Twitter Page of Riyama Ally
  • YouTube of Riyama Ally
  • Website of Riyama Ally
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More