Jane's Journey

Home » Casts » Leah Richard Mwendamseka


Leah Richard Mwendamseka

Other Name/s: Leah Richard Mwendamseka a.k.a Lamata

Actor | Director | Producer

Jina la Lamata si ngeni sana kwa wadau wa filamu hapa nchini, Lamata jina lake halisi ni Leah Richard Mwendamseke katika makala ya leo anapata nafasi ya kuongelea fani yake katika tasnia ya filamu Swahihiliwood, Lamata lizaliwa Jijini Mbeya alipata elimu yake ya Shule ya msingi katika shule ya Ukuti darasa la kwanza hadi la tano.

Leah Richard Mwendamseka a.k.a Lamata

Baadae alihamishiwa shule ya msingi Karobe na kusoma darasa la sita na kumalizia la saba, shule ya Sekondari alisoma Arage kidato cha kwanza na pili huko Mbeya kuhamishiwa katika shule ya sekondari ya Wanging’ombe Mkoani Iringa kidatu cha tano na sita Perfect vision.

Lamata jembe katika tasnia ya filamu Swahiliwood.

Sanaa ya uigizaji alianza rasmi mwaka 2008 katika kikundi cha sanaa cha Amka ambao walikuwa wanarusha michezo yao kituo cha televisheni cha ITV, Lamata akiwa katika kundi hilo aliaanza kama muigizaji na ailiigiza sehemu chache katika mchezo wa Ndoano, baadae aliaanza kuandika script.

“Mnamo mwaka 2009 nikaanza kufanya kazi katika kampuni ya RJ chini ya uongozi wa director VIncent Kigosi ( Ray) kama Production manager,kwa kushirikiana na kampuni hiyo nikaanza kujifunza kazi ya udirector,kuna madirector wengi walionisaidia kama Vicent Kigosi,Selles Mapunda na Adam Kuambiana, pamona msaada kutoka kwa waongozaji tofauti tofauti Ray ndio alinipa msaada mkubwa,”anasema Lamata.

Mwanadada huyo anasema kuwa katika kufunzwa huko hakuishia kupokea mafunzo hayo tu lakini hiyo haikutosha alianza kujifunza zaidi kupitia mitandao mbalimbali inayohusiana na filamu na vile vile kusoma vitabu mbali mbali, Kazi hiyo ilimsaidia kupata urahisi kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wa kuangalia filamu tangu utoto wake, tabaia ambayo ameendelea nayo hadi sasa ya kupenda sana kuangalia filamu hasa za nje ili kujifunza zaidi kwa kuona wenzetu wanafanya nini na sisi tuko wapi.

“Kwa sasa nimekuwa nikijitegemea mwenyewe katika kazi hii ya Uongozaji wa filamu tangu mwaka2010, na nimefanya kazi na makampuni mbalimbali, vile vile nina tunga (story) hadithi na kuandika muswada (script),”anasema Lamata.

Baadhi ya filamu alizoongoza mwanadada huyo ni Candy, All about Love, My Angel,Rude,My Princess,Tears forever, Time after time,Dunia nyingine,House maid,Injinia, na kuweza kuandika baadhi ya miswada katika filamu kama Mke mwema,Mr. President,Chocolate,Life to life,The Avenger,Family war,Injinia.

Lamata kwa sasa anamiliki kampuni yake inayoitwa Lamata Entertainment lakini pamoja na kuwa na kampuni kwa ajili ya masuala ya filamu lakini anashirikiana na kampuni nyingine katika kutengeneza filamu, kama ilivyo sasa anatengeneza filamu ya Injinia chini ya kampuni ya Papa Zi Art Entertainment & Promoters ya jijini Dar es Salaam.

Mwanadada huyo anasema kuwa katika utendaji wa kazi zake katika tasnia ya filamu zipo nyingi sana ikiwa mojawapo Waongozaji kutopewa kipaumbele hadi pale wanapokuwa waigizaji tena wale nyota, lakini kwa jinsi alivyojifunza alihisi anatakiwa kuwa na vitu vichache zaidi katika tasnia ya filamu kuliko kukumbatia kila kitu ili aweze kufanya kazi yake kwa ufaninisi zaidi.

Pia anawashauri akina dada wajitokeze kuwa waongozaji wa filamu au kupiga picha za filamu bila kuhofia watapokelewaje katika tasnia hiyo, na anaiomba Serikali kuisaidia sekta hiyo ambayo anaamini kuwa inaweza kutoa ajira kwa kiwango kikubwa kuliko sekta nyingine kwa hapa Tanzania.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Leah Richard Mwendamseka
  • Twitter Page of Leah Richard Mwendamseka
  • YouTube of Leah Richard Mwendamseka
  • Website of Leah Richard Mwendamseka
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More