Jane's Journey

Home » Casts » Lucas Mhavile ‘Joti’


Lucas Mhavile ‘Joti’

Other Name/s: Lucas Lazaro Mhavile a.k.a Joti

Date/s: 09 July 1982

Actor | Commedian | Singer

Lucas Lazaro Mhavile maarufu kama Joti amezaliwa 9 Julai 1982 katika mkoa wa Morogoro Wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Biro. Joti ni msanii wa kuchekesha na ni mwigizaji wa filamu na michezo ya televisheni kutoka nchini Tanzania.

Lucas Lazaro Mhavile a.k.a Joti

Sanaa yake mara nyingi hufanya na Mpoki ambaye ni mwenzi wake tangu alipoanza shughuli za sanaa. Kwa pamoja wanaitwa “Mpoki na Joti”. Wametengeneza mfifululizo ya filamu za vichekesho kadha wa kadha. Uliomaaru sana ni ule wa Kung Fu Bongo - ambao ndani yake wamecheza na Kingwendu.

Maisha yake ndani ya sanaa
Lucas Lazaro Mhavile maarufu kama Joti alikuwa na kipaji cha kuchekesha tangu alipokuwa mtoto. Alikuwa mchekeshaji maarufu katika vikundi vya maigizo shuleni kwao. Kutokana na yeye kupenda sana kazi hii ya uchechi, baada ya kumaliza shule alijiunga na vikundi mbalimbali vya maigizo kwa ajili ya kujiendeleza na kujitafutia uzoefu zaidi. Joti alianza kujizolea umaarufu baada ya kujiunga na kikundi cha Nyota Ensemble ambacho kilikuwa kikionyesha ucheshi katika kituo cha ITV. Hata hivyo watu wengi hawakuvutiwa sana na jinsi walivyokuwa wanacheza ucheshi huo kwenye kituo cha ITV. Baadaye Joti na Mpoki waliamua kuungana na wasanii wenzake na kuanzisha kundi jipya la ucheshi lililojulikana kwa jina la The Comedy.

Kundi hili lilirusha ucheshi wao kwenye kituo cha Televisheni cha EATV. Kundi hili lilikuja kwa kasi na kumuweka msanii Joti katika chati ya juu kabisa kutokana na umahili wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika vichekesho. Joti ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana nchini Tanzania kwani anauwezo wa kucheza kama mwanamke, mzee kikongwe n.k na kuuvaa uhusika huo na watu wakafurahi. Kutokana na umahili wake huo amekuwa na majina mengi tofauti ya kisanii kutokana kucheza nafasi nyingi katika kundi lake.
[hariri] Vikundi alivyopitia

Joti alipitia vikundi kadhaa vya maigizo kabla ya kujiunga na kundi lake analofanya kazi sasa la Ze komedi. Mwaka 2000 - 2001 Joti alikuwa mwingizaji katika kundi la Nyepenyo, baadaye 2001 - 2003 lijiunga na kundi lingine la Sun rise na 2002 - 2003 alichezea kundi liitwalo Nyota Ensemble. Joti ali-maarufu kama Hami Jay, Da Kiboga, Mzee Simbawanga, Asha Ngedere na Andunje alianza kuhamishia usanii wake kwenye TV baada ya kukutana na rafiki yake kipenzi Mpoki.

Joti aliingia mkataba na kituo cha Televisheni cha ITV na kuanza kucheza michezo ya kuchekesha iliyojulika kama Joti na Mpoki. Kikundi cha Joti anachochezea kwa sasa ni ZE COMEDI, kikundi hiki kinaundwa na wasanii watano ambao ni Joti, Masanja maarufu kama mkandamizaji, Mpoki, Maki Regani maarufu kama Shemeji,

Vituo vya Televisheni alivyopitia
Vituo vya Televisheni alivyopitia kama mchekeshaji maarufu nchini Tanzania ni ITV, EATV na TBC1.

Filmography / Discography


External Links

  • Facebook Page of Lucas Mhavile ‘Joti’
  • Twitter Page of Lucas Mhavile ‘Joti’
  • YouTube of Lucas Mhavile ‘Joti’
  • Website of Lucas Mhavile ‘Joti’
 

More Photos

 
 
 

ABOUT US

BongoCinema.com is a one-stop online shop offering a huge variety of Bongo Movies on DVDs and Videos from Tanzania ...

Read More

HELP CENTRE and FAQ

# How do I make an order? # How long will it take to receive my order? # What Payment Options do I have? # Cancel my order? ...

Read More

Our Products

Action; Adventure; Comedy; Crime; Documentary; Drama; Educational; Family; Fantasy; History; Horror; Musical; Romance; Spiritual...

Read More

Comments /Maoni

John said, "I think I saw one of those bongo movie … you know those movies of the week. ... toa maoni yako kwenye bongo movie...

Read More